SERIKALI imezifunga shule zote za awali, za msingi na sekondari zikiwemo za kidato cha tano na sita kwa siku 30 ili kujikinga na kusambaa kwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 unaoathiri mfumo wa hewa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi huo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Amesema, kuanzia leo Serikali imezuia mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyokuwa ya lazima ikiwemo semina, warsha, makongamano, mikutano mbalimbali ikiwemo shughuli za kisiasa na mikusanyiko ya kijamii kwa mwezi mmoja ili kujikinga dhidi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Serikali pia imesitisha michezo yote inayohusisha mikusanyiko ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, UMISETA, na UMITASHUMTA ili kujikinga na kusambaa kwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Majaliwa ametangaza kuwa Hospitali ya Muhimbili Mloganzila Dar es Salaam na Hospitali ya Mawenzi iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro zitatumika kutunza watu watakaoathiriwa na virusi vya corona.
Amezitaja hospitali nyingine zitakazofanya kazi hiyo kuwa ni Mnazi Mmoja Unguja Zanzibar, Hospitali ya Chakechake Pemba na Kituo cha Afya Buswelu mkoani Mwanza.
Chanzo: Tovuti ya HabariLeo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.