TAMASHA la majaribio lenye lengo la kufanya maandalizi na kujipanga kwa ajili ya tamasha kubwa litakalofanyika mwezi Oktoba limefanyika Jijini Dodoma.
Tamasha la Jiji la Dodoma la Sanaa za Ufundi na Maonyesho lililojumuisha muziki na ngoma za Jadi, Sarakasi na tamthilia limeanza likiwa na matarajio ya kulifanya Tamasha hilo mpaka kufikia mwaka 2023 liwe limechukua sura ya Kimataifa na litakaloadhimishwa kila mwaka Jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa na Afisa Utamaduni wa Jiji la Dodoma, Desdery Kuzenza alipokuwa akizungumza na tovuti hii na kufafanua malengo ya tamasha hili la Jiji la Dodoma.
Aidha, Kuzenza amesema kuwa Tamasha hili linalenga kuonesha wasanii na kazi zao, kutafuta masoko ya kazi za wasanii kupitia vipaji vyao na pia kuwatangaza mbele ya jamii ya kimataifa kupitia kazi na ubunifu wao.
Afisa Utamaduni, Kuzenza amesema mpango huu ulikuwepo kwa muda mrefu, na sasa utekelezaji wake umeanza na wao kama timu ya maandalizi ya tamasha hilo wanashukuru kuwa limekuwa la mafanikio na sasa wajipanga kwa ajili ya Tamasha kubwa la Sanaa za Ufundi na Maonyesho litakalofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.