MAAFISA Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote nchini wametakiwa kutambua uwepo wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika maeneo yao pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mashirika hayo ili malengo yaliyosababisha kuanzishwa kwa mashirika hayo yatimie na kuleta maendeleo nchini.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ramadhan Kailima katika kikao Kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika Novemba 8,2022 Jijini Dodoma.
"Tuna mashirika ambayo yanafanya utekelezaji wake katika maeneo yetu tuhakikishe tunafatilia utekelezaji wake, lakini pia tutumie vikao vilivyopo kuyatambulisha mashirika haya hasa katika vikao vya Madiwani wa Kata zetu ili wao sasa wapeleke taarifa za utekelezaji huo kwa Wananchi", amesema Kailima
Sambamba na hilo Kailima amewataka Maafisa hao kushirikiakiana na Maafisa lishe katika utekelezaji wa afua za lishe zilizopo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutokomeza udumavu wa watoto na kuimarisha lishe bora nchini.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum (WMJJWM), Dr. Zainabu Chaula amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya WMJJWM, amezitaka Wizara hizo kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kutoa mafunzo ya kimkakati kwa Maafisa Maendeleo Jamii nchini yenye lengo la kukumbushana mambo mbalimbali yakiutendaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Bi. Mwantumu Maiza amewataka maafisa hao kuhakikisha wanashirikiana na Maafisa elimu katika kutokomeza ukatili wa kijinsia pamoja na mimba za Utotoni kwa kuandaa vikao shuleni ili kuleta uelewa na kuvunja ukimya wa ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.