SHIRIKA la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) limepata tuzo ya dhahabu miongoni mwa washindi 51 kutoka nchi 39 duniani wa tuzo ya huduma za viwango zinazotolewa na taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR).
Tuzo za ESQR za huduma bora hutolewa kila mwaka na shirika la ESQR kwa kutambua tassisi za kiserikali na zisizo za kiserikali pomaja na watu binafsi wanaotoa huduma za viwango vya juu. Washindi wa tuzo hii huchaguliwa kwa kuzingatia matokea ya kura zilizopigwa na taasisi zilizoshinda tuzo hizi awali, maoni ya wateja na utafiti wa masoko.
Mchakato wa upatikanaji wa washindi wa tuzo hii unajumuishia utafiti wa taarifa mbalimbali za umma, machapisho, maoni chanya ya wateja, miradi ya kijamii na vyuo vikuu pamoja na maonesho.
Tuzo hii ni matokeo ya mikakati madhubuti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania katika kuhifadhi rasilimali pamoja na mrejesho chanya kutoka kwa wateja wa kitaifa na kimataifa. Utambuzi huu utakuwa chachu ya kuendelea kuongeza jitihasa za uhifadhi endelevu wa hidfachi zetu, kutangaza vivutio katika masoko mbalimbali na kuendelea kuboresha huduma za utalii. Ni matarajio kuwa jitihada hizi zitachangia katika kuongeza idadi ya watalii kufikia malengo ya Serikali ya watalii mioni tano ifikapo 2025.
Aidha, Balozi wa Tanzania chini Ubelgiji Mhe. Jestas Nyamanga atapokea rasmi tuzo hiyo mapema wiki ijayo kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania jijini Brussels, Ubergiji.
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania linaendelea kutoa wito kwa umma kwa ujumla, Taasisi za kitaifa na kimataifa pamoja na wadau wa maendeleo kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhifadhi rasilimali za Hifadhi za Taifa na kuunga juhudi za kukuza utalii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.