Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba wakati akikagua kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme wa Gridi ya Taifa, mwishoni mwa wiki (Septemba 17, 2021) amesema atahakikisha TANESCO inakuwa Shirika bora Afrika Mashariki.
Aidha amewataka watendaji wa Shirika kujiandaa kwa mabadiliko makubwa yenye tija yatakayo saidia kuimarisha Shirika ili kuongeza tija na ufanisi.
Mhe. Makamba ameagiza TANESCO kuhakikisha wanatatua matatizo ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo ametoa wiki mbili kwa wataalamu kuhakikisha wanatatua tatizo hilo kwenye maeneo mbalimbali.
Lengo la Mhe. Makamba kufika kwenye kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme wa Grid ya Taifa kilichopo ubungo Dar es salaam, ni kujifunza na kuelewa kuhusu mfumo mzima wa Grid ya Taifa.
Mhe. Makamba amesema Shirika lina mambo mengi ya kufanya kama uwekezaji mbalimbali na kuongeza wateja Nchi nzima ili kuweza kufikia adhima yake yakuwa shirika bora Afrika Mashariki.
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (wa tatu kutoka kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalam wa TANESCO.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.