MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki zoezi la upandaji miti katika barabara za pembeni mwa barabara ya iyumbu kuelekea Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) zinazosimamiwa na TANROAD Mkoa wa Dodoma Leo tarehe 31 Januari 2024.
Akizungumza na wananchi, wanafunzi na watumishi waliojitokeza kushiriki katika zoezi ilo Rc Senyamule amesema TANROAD wametekeleza ipasavyo maagizo ya Makamu wa Rais Dkt . Philip Mpango ambaye amekua akisisitiza juu ya upandaji miti katika Mkoa huo kupitia kampeni ya ‘kijanisha Dodoma’.
Amesema kila mmoja anawajibu wa kupanda miti angalau mitano katika mazingira yanayomzunguka ili kuwezesha mazingira yake kuwa ya Kijani na kutekeleza maagizo ya Viongozi wao.
“Kila mtu anawajibu wakutunza na kupanda miti kwasababu inafaida nyingi katika maisha ya Kila siku ya mwanadamu , tena hakikisheni miti inayopandwa inahudumiwa vizuri ili iweze kukua na kustawi vizuri na sio muishie kupanda tuu mkaitelekeza hakikisheni mnakua na uangalizi mzurii ili tufikie matarajio tuliyojiwekea ya kupendezesha Mkoa wetu,” amesema Senyamule.
Kwa upande wake Menaja wa TANROAD Mkoa wa Dodoma Bi.Zuhura Amani ameahidi na kumuhakikishia Rc Senyamule kuitunza vyema Miti hiyo ili kuhakikisha inastawi vyema na kwa ubora uliokusudiwa ili kuhakikisha Dodoma Inakua ya Kijani Muda wote.
Zoezi la kupanda miti linaendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni kuelekea kilele cha Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwezi April Mwaka huu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.