TANZANIA imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa wa Malaria licha ya baadhi ya mikoa kuwa na maambukizi ya juu ya ugonjwa huo na mikoa ya Arusha, Manyara, Njombe, Kilimanjaro na Iringa kuwa na maambukizi chini ya asilimia moja na mikoa mingine kuwa na maambukizi ya kati.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati akifungua kikao kazi cha kwanza cha wataalamu wabobezi wa kudhibiti wadudu wadhurifu waenezao magonjwa tangu kuanzishwa kwa kitengo cha kudhibiti wadudu wadhurifu hapa nchini.
Dkt. Subi amesema kikosi hicho cha wataalum kinaandaa muongozo wa jinsi ya kukabiliana na wadudu wadhurifu waenezao magonjwa akiwemo mbu. Lengo ikiwa ni kuishauri Wizara njia bora za kukabiliana na wadudu hao.
Alitaja njia hizo ni pamoja na udhibiti wa mazingira kwa kuhakikisha mbu na wadudu wengine wadhurifu hawapati sehemu ya kuzaliana na kuweza kusambaza magonjwa na masuala ya usafi wa mazingira ikiwemo uboreshaji wa nyumba ili kuzuia wadudu wadhurifu pamoja kuhakikisha watu wanalala kwenye vyandarua vyenye dawa.
Kwa upande wa matumizi ya viuatilifu Dkt. Subi alisema katika kudhibiti mbu alitolea mfano vipo viuatilifu na viuadudu vya kuuwa viluilui kwenye mazalia ya mbu, na amesisitiza kutumia viwanda vya ndani kwa kuwa taasisi za ndani ambazo zinafanya tafiti na kuonesha mafanikio makubwa ya idadi ya mbu kupungua pamoja mnyororo wa maambukizi.
“Matumizi sahihi ya vyandarua ni muhimu sana katika kudhibiti Malaria, tunataka angalau zaidi asilimia 80 ya watanzania walalie vyandarua vilivyoweka viuatilifu vya muda mrefu ili kumpunguzia mbu umri wa kuishi na hivyo kupunguza uwezekano wa kusambaza vimelea vya Malaria ikiwa ni pamoja na upuliziaji wa viuatilifu ukoko ndani ya nyumba”.Alisisitiza Dkt. Subi.
Chanzo: Wizara ya Afya (wizara_afyatz) Instagram
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.