*YALIYOJIRI WAKATI WA UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA UZALISHAJI UMEME KATIKA MTO RUFIJI*
*Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli*
#Siku hii ni ya kipekee sana kwa nchi yetu ikiwa tumeanza kutekeleza mradi huu wa ndoto ya mwalimu Nyerere kwani aliamini ni kichocheo cha ukuaji wa sekta zote.
#Kuja kwa wawakilishi kutoka Misri kwa ajili ya kushuhudia tukio hili ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi zetu hizi mbili.
#Ujengaji wa Uchumi wa viwanda kokote duniani ni lazima uwe na uhakika wa umeme na wa bei nafuu, mradi huu ni suluhisho.
#Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni taifa huru na sio masikini, mradi huu ulipigwa vita ndani na nje ya nchi, sasa tunautekeleza kwa pesa zetu wenyewe.
#Mradi huu ni ishara kuwa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunaweza.
#Mradi huu utazalisha umeme mwingi ambao ni mwingi kuliko umeme wote uliozalishwa nchini Tangu tumepata uhuru, tutakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu.
#Mradi huu utasaidia kukuza sekta ya Biashara na uwekezaji nchini hasa kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei nafuu.
#Uwepo wa mradi huu utachochea fursa za Kilimo, Umwagiliaji na Uvuvi kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi.
#Utekelezaji wa Mradi huu pia utasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta ya utalii, wanyama wengi watakuja maeneo haya kunywa maji, utalii wa michezo na wale watakaokwenda kuangalia mitambo ya kuzalishia umeme.
#Ninaagiza kuwa sehemu ya Selous Game Reserve ikatwe na iwe Hifadhi ya Taifa.
#Ninaagiza barabara kutoka Eneo la Fuga mpaka eneo la Mradi ijengwe barabara kwa kiwango cha lami, na tutatumia fedha zilizorudishwa na ndugu yetu Mhe. Rais Uhuru Kenyatta.
#Niwapongeze wote wanaosimamia sekta ya nishati hasa TANESCO na Wizara ya Nishati, mnafanya kazi kubwa sana, hata mgao kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa.
#Mpaka sasa tumepeleka umeme kwenye vijiji 7,419 ambapo ni ongezo la asilimia 254.
#Naombeni sana mkamilishe mradi huu kwa wakati na hata ikiwezekana kabla ya wakati, kwetu sisi pesa sio tatizo.
#Bima ya Mradi huu 100% lazima itolewe na Serikali, Waziri ulizingatie, Wizara ya Fedha mlizingatie, TANESCO mlizingatie, ole wenu mkatafute akasaini bima mtu binafsi.
#Wakazi wanaoishi maeneo haya ndio wawe kipaumbele katika kupatiwa ajira.
#Niwaombe wale wote watakaofanikiwa kupata kazi katika mradi huu, muwe waaminifu, msiibe chochote ili tuukamilishe kwa wakati na kwa ufanisi.
#Bwawa hili likikamilika liitwe BWAWA LA NYERERE, na hata sehemu ya Selous Game Reserve itakayokatwa iitwe NYERERE NATIONAL PARK.
*Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa*
#Ndoto yako leo Mheshimiwa Rais ya kupeleka umeme kwa kila nyumba ya mtanzania mijini na vijijini inakwenda kutimia.
#Watanzania endeleni kuiunga mkono Serikali hii iendelee kuchapa kazi ili kuiletea maendeleo nchi yetu.
*Naibu Spika wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson*
#Sisi kama wawakilishi wa wananchi Bungeni tunakupongeza sana kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huu.
*Waziri wa Nishati wa Tanzania Dkt. Medard Kalemani*
#Nakupongeza kwa kutekeleza mradi huu, nina kuahidi kuusimamia, huu ni mradi kwa kwanza kusimamiwa na watanzania.
# Umeme huu utasafirishwa kutoka Rufiji kwenda Chalinze, Dar halafu Dodoma na ndio umeme utakaotumika katika kuendesha Treni ya Mwendokasi.
#Mradi huu ni moja ya utekelezaji wa ahadi kwa nchi kuzalisha Megawati 10,000 kufikia mwaka 2025.
#Mradi huu ni chachu katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini.
*Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohammed Shakkah*
#Mradi huu unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TANESCO na makampuni mawili ya Misri ni moja ya hatua kubwa ya mahusiano kati ya Tanzania na Misri.
#Mradi huu utasaidia Tanzania kuzalisha umeme wa kutosha na kutekeleza Malengo ya Milenia ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.
#Mradi huu utawezesha Nchi ya Tanzania kuzalisha umeme wa kutosha na hata kuwa na uwezo wa kuzisaidia nchi jirani.
#Misri tutatoa nafasi 50 za mafunzo kwenye sekta ya Nishati kwa Watanzania.
*Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka*
#Gharama ya Mradi huu ni Tsh Tril. 6.5 na mpaka sasa tumeshalipa 15% ya gharama hiyo ambayo ni TSh Tril 1.007.
#Mhe. Rais tunao umeme unaojitosheleza lakini kukamilika kwa mradi huu kutatuongezea ziada ya umeme utakaotusaidia kutekeleza kwa vitendo azma ya nchi kuelekea uchumi wa kati.
*Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe*
#Mheshimiwa Rais nakupongeza kwa kutimiza ndoto hii ya Baba wa Taifa.
*Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo*
#Utekelezaji wa mradi huu ni moja ya suluhisho ya mafuriko yaliyokuwa yanatokea mara kwa mara kutokana na kufurika kwa Bonde la mto Rufiji.
#Tangu kuanza kutekelezwa kwa mradi huu, wananchi takribani 558 wameajiriwa kutoka maeneo ya Rufiji na Kibiti.
#Kutekelezwa kwa Mradi huu ni chachu ya kukua na kuendelea kwa sekta ya uwekezaji katika Mkoa wetu.
#Tumejipanga kuanza kilimo cha Michikichi, Mpunga na Miwa kutokana na kutekelezwa kwa mradi huu.
Chanzo: Idara ya Habari - MAELEZO
Taarifa ya Ikulu: Taarifa ya Ikulu: Dkt. John Magufuli aweka jiwe la msingi mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.