OR-TAMISEMI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro, amesema kuwa mashindano ya michezo ya Shule za Msingi na Sekondari yanayofanyika nchini kila mwaka ni ya mfano Duniani.
Dkt.Ndumbaro amesema hayo wakati akifungua rasmi mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yanayofanyika kitaifa Mkoani Tabora.
Waziri Ndumbaro ameeleza kuwa ukubwa wa mashindano hayo unepelekea kupokea pongezi kutoka shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA,ambayo kwa mara ya kwanza imetuma wataalam wake kufuatilia vipaji kupitia michezo ya mwaka huu.
"FIFA wametuma wawakilishi ambao ni wataalam wa ufundi kushuhudia mashindano haya, wengine walikuwepo wakati wa UMITASHUMTA na leo wanaingia wengine kuongeza nguvu kwa ajili ya UMISSETA, huu ni ushahidi kuwa michezo hii ina thamani kubwa"
Dkt.Ndumbaro ameelezea maboresho makubwa ya mashindano ambayo yameendelea kufanyika kuwa ni kutokana na Serikali ya awamu ya sita kuendelea kuipa thamani michezo nchini hususani kwenye ngazi ya shule za msingi na sekondari.
"Juhudi hizi za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan zinapaswa kuungwa mkono na wadau wengine wa michezo nchini, kwa sababu michezo ni ajira ambayo inatakiwa kuandaliwa kuanzia katika ngazi ya chini"
"Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Elimu tunakuja na kauli mbiu isemayo "Michezo ni ajira Michezo ni Uchumi" inayolenga kukuza michezo nchini.ameeleza Dkt.Ndumbaro
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.