Rais John Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda leo Septemba 13, 2020 wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga
Rais Magufuli amesema hatua hiyo ni ya muhimu sana kuelekea utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya takriban Dola za Marekani Bilioni 3.5
Ameongeza kuwa, hapa nchini bomba litapita kwenye Mikoa 8, Wilaya 24 na Kata 132. Aidha, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia inayokadiriwa kufikia Bilioni 21
Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni akisema amefanya mambo yasiyowezekana na endapo mafuta hayo yasingepatikana Uganda, Tanzania isingenufaika Rais Magufuli ameongeza kusema kuwa mradi huo utaimarisha uchumi wa nchi hizo na eneo lote la Afrika Mashariki na Kati.
Rais Museveni alisema kitu muhimu ni kuanza kwa mradi huo aliosema ulicheleweshwa kutokana na mlipuko wa COVID-19.
Aidha, Viongozi hao wawili wamekubaliana asilimia 60 ya faida ya itakayopatikana katika mafuta hayo itakwenda kwa Tanzania huku asilimia 40 ikienda kwa Uganda.
Viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.