WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amesema hadi kufikia Aprili 30, 2022 jumla ya anwani za makazi 12,171,320 zimekusanywa na kuingizwa kwenye Program tumizi ikiwa ni sawa na asilimia 104.3 ya lengo la jumla ya Anwani 11,676,891 zilizopangwa kukusanywa katika Mkoa yote nchini.

Ameyasema hayo leo Mei 20, 2022 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha ya Wizara hiyo.
Nape amesema kufuatia malengo ya Serikali ya kukamilisha Anwani za Makazi kabla ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Mwezi Agosti, 2022, katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kilichofanyika tarehe 08 Februari, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alielekeza Mfumo wa Anwani za Makazi kutekelezwa kwa Mfumo wa Operesheni, aliyoipa jina la ‘OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI’.
“Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Ofisi ya Rais – TAMISEMI zimeendelea na utekelezaji wa Mradi chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu” amesema Mhe. Nape.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22 shughuli nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na kuunda program tumizi (Mobile application) ya mfumo iliyoongeza ufanisi katika matumizi na utekelezaji wa mfumo na kuongeza kuwa program hiyo imetumika katika kukusanya taarifa za barabara, mitaa, njia, makazi na wakazi sambamba na kumuongoza mtu kutoka anwani ya makazi moja kwenda anwani ya makazi nyingine.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.