TANZANIA imepanda kwa nafasi tisa kutoka kutoka ya 97 hadi ya 88 duniani huku ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki.
Vilevile imeshika nafasi ya tatu katika nchi za kusini ya jangwa la Sahara. Nchi hii imepanda hadi nafasi ya tisa ikilinganishwa na ripoti kama hiyo mwaka jana.
Katika ripoti ya jarida la Global Innovation Index ya mwaka huu, lililofanya utafiti Julai mwaka jana hadi Juni, mwaka huu kabla ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, nchi hii imepanda hadi nafasi ya tisa ikilinganishwa na ripoti kama hiyo mwaka jana.
Jarida hilo la Global Innovation Index hutolewa na World Intellectual Property Organization, WIPO.
Pamoja na hayo, kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya tatu katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na pili katika nchi za Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
Kenya mwaka huu, imeshika nafasi ya 10 katika nchi zenye uchumi wa kati ikishika nafasi ya 86 kati ya nchi 131 zilizofanyiwa utafiti duniani.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa katika nchi hizo za uchumi wa chini, Tanzania imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya pili na Nepal iliyoshika nafasi ya tatu.
Kwa nchi za Afrika Mashariki, pamoja na Kenya iliyoshika nafasi ya 86, Rwanda ilishika nafasi ya 91 na Uganda nafasi ya 114. Kwa kuzingatia nafasi hizo Tanzania ni ya pili Afrika Mashariki kwa ubunifu.
Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo kwenye nchi za Jangwa la Sahara, Tanzania ilishika nafasi ya tatu kwa ubunifu wa kiuchumi, ikitanguliwa na Afrika Kusini iliyoshika nafasi ya kwanza na Kenya iliyoshika nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inayotolewa kila mwaka ikiangalia ubunifu wa nchi katika kukuza uchumi, mwaka huu Tanzania imeingia pia katika nchi 41 ambazo maendeleo yake yako kiwango cha juu cha matarajio ya utafiti huo.
Historia ya ripoti hizo kwa miaka mitatu zinaonesha nchi hiyo imekuwa ikipanda na kushuka katika eneo la ubunifu wa uchumi ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya 96, mwaka 2018 nafasi ya 92, mwaka jana nafasi ya 97 na mwaka huu imeshika nafasi ya 88 kati ya nchi 131 zilizofanyiwa utafiti.
Aidha, ripoti hiyo ya Global Innovation Index ya mwaka huu, ilieleza kuwa maeneo yaliyopimwa kwa ubunifu katika nchi hizo 131 ikiwemo Tanzania ni ubunifu katika miundombinu, mapato katika maarifa na teknolojia, mitaji ya binadamu na utafiti.
Maeneo mengine ni matokeo ya ubunifu, taasisi, uboreshaji wa biashara, uboreshaji wa masoko ambayo tangu mwaka jana ripoti hiyo imeonesha kuwa Tanzania inayatekeleza vizuri kiubunifu.
Pamoja na hayo, katika ripoti hiyo ya mwaka huu, imeitaja Uswizi kuwa nchi ya kwanza duniani kwa ubunifu ikifuatiwa na Sweden na Marekani. Huku nchi tatu za mwisho kwa ubunifu ni Yemen, Guinea na Myanmar.
Chanzo: HabariLeo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.