UBALOZI wa Tanzania nchini Uturuki umeratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 3 wa Kongamano la Biashara kati ya Afrika na Uturuki unaofanyika kwa siku 2 Jijini Istanbul nchini Uturuki kuanzia leo tarehe 21 mpaka 22 Oktoba 2021.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameambatana na Mheshimiwa Shaaban Omar Saïd (Mb) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Mheshimiwa Daniel David Mwakiposa, Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara zaidi ya mia moja kushiriki mkutano huo.
Mkutano huo unalenga kufungua fursa zaidi za ushirikiano kati ya Afrika na Uturuki katika sekta za viwanda na biashara.
Ujumbe wa Tanzania umewasili jana tarehe 20/10/2021 na kupokelewa na Bwana Hassani Iddi Mwamweta, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki. Ikumbukwe Uturuki na Tanzania wamekuwa na uhusiano mzuri na wa kihistoria uliojikita katika sekta za Uwekezaji , biashara, elimu, afya pamoja na Miundombinu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.