WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania imewasilisha miradi minane yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.334 katika Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaohudu ushirikiano wa Maendeleo baina ya Japan na Afrika (TICAD8) ambao umemalizika jana tarehe 28 Agosti 2022.
Miradi iliyowasilishwa ni ya ukarabati wa barabara ya Morogoro – Dodoma kwa kiwango cha lami, mradi wa umwagiliaji katika bonde la Ziwa Victoria, mradi wa kusambaza maji Lugoda (Mufindi), kujenga uwezo wa kituo cha utafiti cha ufugaji wa samaki Dar es Salaam, bandari ya kisasa ya uvuvi, kuanzisha maabara ya kuthibitisha ubora kwenye sekta ya uvuvi na ukarabati wa bandari ya uvuvi ya Wete na ujenzi wa njia ya umeme ya Somanga-Fungu-Mkuranga.
Akizungumza leo (Jumatatu, Agosti 29, 2022) jijini Tunis, Tunisia, ambako alikuwa akimwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa TICAD.
“Kupitia mikutano ya TICAD, sisi tumenufaika na ujenzi wa daraja la Mfugale, mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi II, na sasa tumeomba watukamilishie miradi mitatu ya barabara ya Arusha-Holili, Bandari ya Kigoma na mradi wa maji wa Zanzibar,” amesema.
Miradi mitatu ambayo imeombewa fedha inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 343.8 ambapo kati ya hizo dola za Marakani milioni 221 ni kwa ajili ya mradi wa barabara ya Arusha-Holili, dola milioni 98.7 (mradi wa kuboresha miundombinu ya usambazaji wa maji Zanzibar) na dola milioni 24.1 (bandari ya Kigoma).
Kuhusu sekta ya kilimo, Waziri Mkuu amesema kupitia TICAD 8, Tanzania imeomba kupewa kipaumbele ili iweze kuongeza wigo wa kilimo. “Tunahitaji kuhakikisha tuna chakula kingi ili tuwe na ziada na tuweze kuuza nje ya nchi” alimalizia Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu pia alifanya mkutano na viongozi wa kampuni ya Japan Tobacco Incorporation (JTI), Mitsubishi na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Japan (JICA).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.