KATIKA kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongzwa na Mhe. Samia Suluhu Hassn, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanafikiwa, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), imepanga mwaka huu kufanya tafiti mbili kubwa ambazo zitajikita kwenye kubaini nguvu kazi Pamoja na rasilimali watu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo leo tarehe 27 Mei, 2021, Jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wanaendelea kushirikiana ambapo Wizara hiyo inapitia sera ya elimu nah uku Ofisi hiyo ikifanya tafiti.
“Mwaka huu tumeamua kufanya tafiti mbili kubwa ambapo tafiti moja tunaendelea nayo ambayo ni hali ya nguvu kazi nchini. Utafiti huo utatusaidia kujua ni asilimia ngapi ya vijana wanaofundishwa ndani ya nchi na wanaweza kuajirika nchini na kama hawaajiriki ni kwa nini. Aidha, Utafiti huo utatusaidia kuelewa sekta ipi yenye fursa nyingi kuliko sekta nyingine ya ajira, hii itasaidia mafunzo ya ufundi yaendane na mahitaji yetu ya ajira” Amesisitiza Mhagama.
Vile vile, Mhe. Mhagama amefafanua kuwa Serikali imeshakamilisha utaratibu wa kufanya utafiti wa Hali ya Rasilimali watu nchini. Utafiti huo utasaidia kuelewa juu ya Watanzania waliopo nchini na waliopo nje ya nchi kama wanaendan na mahitaji wa ajira kwa sasa.
Ameongeza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikisimamia vibali vya ajira kwa wageni, hivyo wataelewa sababu ambazo hupelekea wawekezaji kuhitaji kuwaleta watu wao wenye ujuzi ilhali wenye ujuzi wa viwango hivyo wapo hapa Tanzania, lakini pia itaeleweka maeneo gani ambayo nchi haina ujuzi na wangependa ujuzi huo upatikane hapa nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.