• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

TEHAMA chachu ya ukusanyaji mapato Dodoma Jiji

Imewekwa tarehe: March 27th, 2024

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

MATUMIZI ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yamerahisisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi na kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Fungo alisema “matumizi ya TEHAMA yamerahisisha sana shughuli za serikali za kutoa huduma kwa wakati na kwa urahisi kwa wananchi. Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Halmashauri ya Jiji la Dodoma upatikanaji wa fedha kwenye ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA ikiwemo mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam ili wawe na uelewa wa kutosha kuweza kufanyia kazi mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA kwa wakati”.

Akiongelea mafanikio katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA, alisema kuwa mifumo imeleta mapinduzi makubwa. “Mfumo wa kukusanya mapato Tausi umesaidia katika ukusanyaji wa mapato. Halmashauri ya Jiji vyanzo vyake vyote vya mapato vimeingizwa katika mfumo wa Tausi na kukusanywa kieletroniki na hivyo, kuondoa mianya ya upotevu fedha za Serikali. Kupitia TEHAMA tunaweza kufahamu mapato halisi ambayo halmashauri inayapata na kuthibiti upotevu wa fedha na kuwafanya watumishi kuwa makini katika maeneo yao ya ukusanyaji wa mapato. Kupitia mfumo wa Tausi mwananchi anaweza kukata leseni ya biashara, vileo na leseni mbalimbali kwenye mfumo akiwa nyumbani au sehemu yake ya biashara kwa kupitia simu yake ya mkononi” alisema Fungo.

Akiongelea mfumo wa huduma za Afya GOTHOMIS, alisema kuwa unatumika katika vituo vya Afya na zahanati za serikali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Mfumo umesaidia kuongeza usiri wa taarifa za mgonjwa, kuweka kumbukumbu sahihi za taarifa za mgonjwa, kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato, kupunguza foleni na usumbufu usio wa lazima. Kwa mfano, katika Kituo cha Afya Makole tangu tumeanza kutumia mfumo wa GOTHOMIS kituo kilikuwa kinakusanya shilingi 12,000,000 kwa mwezi. Baada ya kuanza kutumia mfumo mapato yalipanda hadi shilingi 36,000,000 kwa mwezi. Hivyo, mfumo ulitusaidia sana kudhibiti upotevu mapato na kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi kwa sababu ya urahisi wa kutumia mfumo huu” alisema Fungo.

Wakati huohuo, alisema kuwa halmashauri imejipambanua sana kwenye matumizi ya TEHAMA kufikisha habari kwa wananchi. “Tunahakikisha sisi wenyewe tunakuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa wananchi kupitia mitandao ya kijamii. Mfano tovuti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma www.dodomacc.go.tz tumekuwa tukiweka habari na taarifa mbalimbali za maendeleo na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na mrejesho kutoka kwa wananchi. Pia tunazo kurasa za mitandao ya kijamii kwenye Instagram, Facebook na Youtube channel inayofahamika kama Dodoma City Tv” aliongeza.

Kitengo cha TEHAMA kina jukumu la kusimamia mifumo, miundombinu, data na vifaa vya TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli za kila siku za Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.