NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu , Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutenga fedha kupitia mapato ya ndani na kujenga mabweni katika shule za kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Katimba ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Ofisi ya Rais – Tamisemi wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Regina Qwaray aliyetaka kujua kuna mkakati wa serikali kuhakikisha Shule zote za Sekondari nchini zinajengewa Mabweni.
Akijibu swali hilo amesema “Naomba kuwakumbusha wakurugenzi wote kuhakikisha kwamba katika mapato yao ya ndani wanatenga fedha kwaajili ya kujenga mabweni ya kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne aidha, Serikali itaendelea kuweka kipaumbele katika ujenzi wa Mabweni kwenye shule za Sekondari za kidato cha Tano na Sita nchini ili kuwawezesha Wanafunzi wote wanaofaulu mtihani wa kidato cha Nne waweze kupata fursa ya kujiunga Kidato cha Tano”.amesema Zainab Katimba
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.