Madaktari bingwa na Wataalam wa magonjwa ya Sikio, Pua na Koo nchini (TENT) wameahidi kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kuanzisha huduma za upandikizaji wa Kifaa Maalumu cha Usikivu (Cochlear Implant) ili kuwasogezea huduma hiyo wananchi wa Kanda ya Kati.
Awali akifungua mkutano wa mwaka wa kisayansi wa Jumuiya ya Madaktari bingwa na Wataalam wa magonjwa ya Sikio, Pua na Koo unaoendela katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Januarius Hinju, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ametoa rai kwa wataalamu hao kutumia mkutano huo ili pamoja na mambo mengine wajadili namna bora ya kushirikiana kutoa huduma ya kupandikiza kifaa maalumu cha Usikivu (Cochlear), ili kuwapunguzia wananchi wa kanda ya kati usumbufu wa kufuata huduma hiyo Dar es Salaam
“kwa vile tumebobea katika huduma za kupandikiza viungo, na tuna vifaa vya kisasa kwa matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya masikio, pua na koo, tunawaalika wataalamu wazawa wa magonjwa ya Sikio, Pua na Koo waje tushirikiane kutoa huduma za kibingwa za kupandikiza kifaa maalum cha usikivu, alisema Dkt. Hinju.
Aidha, Dkt. Hinju amebainisha kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa inazidi kuboresha huduma zake kwani ndani ya kipindi cha miaka mitano imeweza kutoa huduma za kupandikiza Figo kwa kutumia watalaam wazawa na kwa sasa iko mbioni kutoa huduma za upasuaji moyo kwa kufungua kifua (open heart surgery) pamoja na kupandikiza uroto.
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madaktari bingwa na Wataalam wa Magonjwa ya Sikio, Pua na Koo (TENT) Dkt. Edwin Liyombo ameishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa mapokezi makubwa waliyopata na kuahidi kutumia mkutano huo kulifanyia kazi ombi la kushirikiana kutoa huduma za kibingwa za kupandikiza kifaa maalum cha usikivu kwa wananchi wa Kanda ya Kati.
“Kabla ya Mkutano huu nilikuja kutembea hapa BMH, hii hospitali iko vizuri, inavifaa vya kisasa kabisa, hata vifaa tiba vinavyotumika kwenye kliniki za ENT ni vya viwango vya kisasa vinavyotumika katika hospitali za Ulaya, TENT nchini tupo tayari kushirikiana nanyi wakati wowote” Alisema Dkt. Edwin.
Picha na matukio:
Chanzo: Wizara_afyatz
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.