KATIKA kuendeleza soka la Tanzania na kufikia hadhi ya kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) limesaini mkataba na kampuni ya Group Six International Ltd ili kujenga vituo bora vya mpira hapa nchini.
Zoezi hilo la kusaini makubaliano hayo ya ujenzi wa vituo hivyo lilifanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2020 katika ofisi za TFF likitanguliwa na zoezi kama hilo lililofanyika Jijini Tanga tarehe 29 Septemba, 2020.
Makubaliano hayo yamelenga mradi huo utakaotekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Kigamboni, Kigamboni Technical Center, pamoja na Mkoani Tanga, Tanga Technical Center.
Mradi huo utajengwa kwa kutumia fedha za FIFA na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12, mara baada ya kuanza kwa ujenzi huo.
Aidha Rais wa TFF Wallace Karia alisema kuwa miradi hiyo inakwenda kwa awamu na matarajio yake ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na vituo hivyo vya mpira.
"Mradi unakwenda kwa awamu, na katika mipango yetu tutahakikisha kila Mkoa unakuwa na kitu kama hicho, tutatumia fedha za wadau wetu mbalimbali pamoja na wale watakaojitokeza pia." Amesema Wallace Karia.
Mwonekano wa Kituo cha Michezo cha Kigamboni kitakapokamilika.
Mwonekano wa Kituo cha Michezo cha Tanga kitakapokamilika.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia akimuonyesha mwakilishi wa kampuni ya Group Six International Ltd eneo la mradi wa ujenzi wa Kituo cha Michezo Kigamboni.
Rais wa TFF Wallace Karia (wa pili kulia) na Mkandarasi Yi Xiaobo (wa tatu kulia) wa kampuni ya Group Six International wakionesha mikataba ya ujenzi wa vituo vya mpira wa miguu vya Dar es Salaam na Tanga uliosainiwa Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.