Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kati yatenga kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuhudumia miti iliyopandwa Jijini Dodoma katika kampeni ya kukijanisha Dodoma iliyozinduliwa mwaka 2017.
Akizungumza ofisini kwake Meneja wa TFS Kanda ya kati Mathew Kiyondo amesema kuwa wametenga fedha hizo ili kuhakikisha miti iliyopandwa inahudumiwa na kukua vizuri hususani katika umwagiliaji na palizi kwani miti hiyo ikikua italeta mandhari na hali nzuri ya hewa Jijini hapa ikiwa ni pamoja na kuondokana na ukame.
Kiyando amesema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kupendezesha madhari ya Jiji la Dodoma kwa kupanda miti mipya na kuitunza iliyokuwepo kwani Halmashauri ya Jiji inamiliki ardhi na wao kama TFS wanamiliki wataalamu pamoja na miti hivyo ushirikiano baina yao unaweza kuzaa matunda na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Akizungumzia changamoto zinazoikabili kampeni hiyo kuwa ni pamoja na maji hasa katika kipindi ambacho mvua hazinyeshi, majanga ya moto ambapo watu wamekua wakichoma moto maeneo jirani hivyo kufanya moto kuhamia katika maeneo yaliyopandwa miti, na mifugo kuvamia maeneo yaliyopandwa miti, changamoto ambazo wameanza kuzitatua na wamefanikiwa kuokoa asilimia 70 ya miti iliyokua kwenye hatari ya kufa.
“Tumetenga kiasi cha shilingi milioni mia moja kwaajili ya kuhakikisha miti iliyopandwa inakua vizuri, lakini pia tumepanga kuweka matanki 18 ya maji ya lita elfu kumi ambayo yatawekwa katika taasisi kama vile shule na kadharika, na tunawashukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma wanatupatia boza la maji ambalo limekua likirahisisha zoezi la umwagiliaji”, Alimalizia Kiyando.
Athali za uharibifu wa moto kwenye mazingira eneo la Medeli.
Meneja wa TFS Kanda ya kati Mathew Kiyondo alipokuwa akizungumza na mwandisi wetu (hayupo pichani) juu ya changamoto na mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa Kukijanisha Dodoma.
Miti iliyostawishwa na kupandwa katika Shule ya Wasichana ya Msalato. Tukiitunza miti yetu itatupa faida nyingi katika jamii yetu na mazingira.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.