• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

THBUB yaiasa Jamii kutofumbia macho vitendo vinavyotweza utu wa mwanawake

Imewekwa tarehe: March 8th, 2021

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeitaka jamii kuendelea kubeba jukumu la kutokuyafumbia macho matukio yote yenye kutweza utu wa mwanamke na kutoa taarifa katika mamlaka husika pindi wanaposhuhudia matukio hayo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani aliyoitoa leo Machi 8, 2021.

Jaji Mwaimu amesema kuwa ni vyema jamii ikaendelea kuhamasishana kuacha mitazamo potofu ya kumchukulia mwanamke kama chombo dhaifu kisichoweza kuleta matokeo chanya ya uongozi ili kujenga jamii yenye usawa.

“Kupitia jitihada mbalimbali za uhamasishaji zilizofanyika nchini kumekuwepo na ushiriki wa wanawake katika masuala ya uongozi kwenye vyama vya siasa, Serikali, Bunge, Mahakama na katika nafasi nyingine za uongozi katika jamii,’” alisema Mwaimu

Ameongeza kuwa pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali za kukemea vitendo vya ukatili kwa wanawake bado kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake katika kuwania nafasi za uongozi zikiwemo mila na desturi zinazominya haki za wanawake, elimu na kipato duni kwa wanawake wenye nia ya kugombea uongozi na kutojiamini.

Mwaimu ameendelea kusema kwa kuwa Serikali  imeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kimataifa inayotoa haki kwa kila mtu kushiriki katika nafasi ya uongozi na utawala wa nchi kwa usawa wa kijinsia, Tume inaunga mkono dhamira hiyo ya Serikali  na kuwahamasisha wanawake kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

“Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikiwahimiza wanawake kuendelea kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi za kijiji/mtaa hadi taifa na kuwajengea uwezo wa namna ya kudai haki zao kisheria pale wanapohisi haki hizo kuvunjwa,” alifafanua Mwaimu

“Hivyo katika maadhimisho ya siku hii muhimu, Tume inaungana na jamii na wadau mbalimbali duniani kutambua mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo,” aliongeza

Jaji Mwaimu alisema kuwa kupitia Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu 2021 ambayo ni ‘Wanawake katika Uongozi: Chachu kufikia Dunia yenye Usawa’,  Tume inaihamasisha jamii yote kuendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha kwamba ushiriki wa wanawake katika uongozi unaongezeka ili kufikia dunia yenye usawa.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.