OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeanza kupokea shilingi Bilioni 22 kutoka Wizara ya Fedha na Mipango zitokanazo na tozo ya Mawasiliano na fedha hizo zinakwenda kujenga vituo vya Afya 90 kwenye Halmashauri 82 nchini.
Fedha hizo zimepelekwa kwenye maeneo ambayo hayana kabisa Kituo cha Afya kwenye Tarafa 90 kati ya 207 ambazo hazina kituo cha afya kabisa.
Aidha, shilingi Bilioni 15 zitakazopelekwa juma hili kutoka Wizara ya Fedha, zitapelekwa kujenga Vituo vya Afya 60 hivyo kufanya jumla ya vituo 150 kujengwa kupitia tozo ya mawasiliano.
Fedha hizi zinakwenda kwa maelekezo maalumu, kuwa Vituo vya Afya vijengwe kwenye Tarafa ambazo hazina vituo vya afya au vilivyopo havina uwezo wa kufanya upasuaji wa dharura.
Tanzania Bara ina jumla ya Tarafa 570 na mpaka hivi sasa Tarafa 207 hazina Vituo vya Afya hivyo kutokana na fedha za Tozo ya Mawasiliano tutajenga vituo vya afya kwenye Tarafa 150 na kubakia na Tarafa 57 tu ambazo zitakuwa hazina vituo vya afya.
Chanzo: ortamisemi (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.