Jumla ya miradi yenye thamani ya Shilingi Trilioni 2.9 sawa na Dola za Marekani Bilioni 1.108 inatekelezwa maeneo mbalimbali nchini Tanzania ikiwa ni adhma ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia katika uendelezaji na uboreshaji wa Miji ili kuhakikisha utoaji bora wa huduma kwa wananchi nchini Tanzania.
Miradi hiyo inayosimamiwa na OR-TAMSMI na kutekekezwa na TARURA kupitia kikundi kazi cha uratibu wa miradi “projects coordiination team (PCT) “ ni mradi wa Uboreshaji Jiji la Dar es Salaam
awamu ya pili (DMDP2) na uendelezaji wa bonde la Mto Msimbazi Mkoani Dar es Salaam pamoja na mradi wa TACTIC unaotekelezwa kwenye miji 45 nchi nzima.
Lengo la miradi hiyo ni kuboresha na kuendeleza huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii ambapo leo Disemba 05, 2024
kumeshuhudiwa utiaji saini wa ujenzi wa kituo cha Mabasi Inala pamoja na soko la Mjini Kati katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora.
Wakati wa utiaji saini mkataba huo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba amesema ni matarajio ya Serikali kuwa miradi hiyo italeta mabadiliko chanya#
kwa wananchi wa Tabora kwani miradi hiyo inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara na kuongeza thamani ya maeneo husika na hivyo kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja na la Mkoa kwa ujumla.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.