VIONGOZI wa Dini Mkoani Dodoma wamewaomba waumini wao na Watanzania wote kwa ujumla kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu hapo kesho.
Hayo yamesemwa leo na Viongozi hao wa imani walipokutana na kutoa kauli hiyo kwa pamoja kuelekea Uchaguzi mkuu wa Tanzania. Aidha wamewasihi Watanzania kurejea nyumbani mara tu baada ya kutekeleza jukumu lao la kikatiba la kupiga kura.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akielezea jinsi Jeshi hilo lilivyojipanga amesema kuwa usalama wa raia na mali zao umeimarishwa mkoani hapa.
Muroto amefafanua kuwa Jeshi la Polisi litashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Mgambo, Magereza, Zimamoto, Uhamiaji na wengineo kuhakikisha amani na usalama ili wananchi wapige kura kwa utulivu na amani.
"Tayari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ametuwezesha kupata usafiri kwa ajili ya kufanya doria na kusafirisha vifaa mbalimbali vitakavyotumika kwenye uchaguzi huo kutoka sehemu moja kwenda nyingine". Amefafanua Muroto.
Aidha, Kamanda Muroto amebainisha kuwa kila kituo kidogo cha kupigia kura kitakuwa na askari, amabo wote kwa pamoja watakutana sehemu kuu ya majumuisho ili kuhakikisha usalama unaimarika wakati wote wa zoezi za uchakuzi katika maeneo yote.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.