WANANCHI wametakiwa kuchagua viongozi bora watakaokuwa chachu ya maendeleo nchini katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Stella Ikupa alipomuwakilisha Waziri wa Sheria na Katiba katika kilele cha maonesho ya 27 ya Nanenane yaliyofanyika kwa Kanda ya Kati jijini Dodoma.
Ikupa alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yaliongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Kwa maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi, chagua kiongozi bora 2020’. “Tunaposema maendeleo, maendeleo hayaji hivihivi, maendeleo yanategemea uongozi bora, pasipo kuwa na uongozi bora, hakuna maendeleo. Mambo yote ya maendeleo ambayo yamekuwa yakitokea katika nchi yetu ni matokeo ya uongozi bora tuliona nao. Kwa hiyo, tukilijua hilo, wajibu wetu ni kuendelea kuchagua viongozi wazuri ambao wataendelea kutupeleka mbali zaidi katika nyanza zote za kiuchumi” alisema Ikupa.
Naibu waziri huyo aliwataka watanzania kudumisha amani, na mshikamano. “Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu lazima kama Watanzania tuweze kuendelea kudumisha amani, mshikamano na uzalendo wetu. Sifa ya Mtanzania ni uzalendo. Unapokuwa Mtanzania lazima uweke uzalendo mbele hata kama kuna nafasi unakuwa unaihitaji lazima utangulize uzalendo kwanza. Lazima tumtangulize Mungu katika yote kama Taifa” alisisitiza Ikupa.
Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yalihudhuriwa na makampuni 31, wajasiriamali zaidi ya 300, taasisi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali wa kilimo, mifugo na uvuvi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.