RAIS Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu ili wananchi waweze kuwapima kutokana na sera watakazonadi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020.
Rais Dkt. Mafuguli ameyasema hayo wakati akizindua jengo la ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo.
Rais Dkt. Magufuli amesema “hili ndilo jengo letu na tutakuja kuchukulia fomu hapa lakini mnaweza kuacha na kusema kuwa Magufuli amepita. Niwaombe sana ndugu zangu wanasiasa wenzangu kama ambavyo imekuwa kawaida yetu,niwaombe uchaguzi huu uwe 'special' kwa kufanya kampeni zetu kwa upole, kumtanguliza Mungu, kujua sisi ni Taifa la Tanzania, na kujenga umoja wa Taifa letu. Tunadi sera zetu na wananchi waweze kutupima kutokana na sera zetu”.
Rais Dkt. Magufuli ameongeza “Mimi ni mwenzenu na tunajenga nyumba moja. Sisi sote na vyama vyote tukimtanguliza Mungu tutafanya vizuri”. Amesema kuwa kwa kufanya hivyo uchaguzi mkuu utakuwa mzuri na huru.
Wakati huohuo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa katika vyama vya siasa hakuna chama kidogo. Aidha, alivitaka vyombo vya dola kutokutumia nguvu kupita kiasi maeneo yasiyostahili kutumiwa nguvu.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.