Na. Mussa Chibukwe, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka wakandarasi waliokabidhiwa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa na vyoo kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya Taifa na siyo kwa manufaa yao binafsi.
Shekimweri aliyasema hayo alipotembelea na kukagua Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Matumbulu.
"Nitoe maelekezo kwa mafundi mfanye kazi kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa mkizingatia kuwa shule tayari zimeshafunguliwa japo kuna wazazi bado wanajivuta katika kukamilisha baadhi ya mahitaji kwa watoto, lakini isiwe sababu ya ujenzi
kutokukamilika kwa wakati. Kwahiyo miradi yote iongezewe kasi katika utekelezaji na ikamilike ndani ya wiki moja kwa ile iliyo katika hatua ya umaliziaji japo kuna changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa miradi" alisisitiza Alhaj Shekimweri
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.