Tume ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 13 Septemba 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa Wasimamizi mbalimbali wa Uchaguzi nchi nzima.
Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.
Aidha, chini ya kanuni ya kanuni ya 30 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2020, Tume inaweza kukubali au kukataa rufaa hizo.
Katika kikao hicho, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 49 za Wagombea Udiwani, kama ifuatavyo:-
Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Udiwani zilizotolewa uamuzi kufikia 244. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume. Imeeleza taarifa ya Tume kwa umma kuhusu uamuzi wa rufaa za wagombea Udiwani iliyotolewa leo tarehe 14 Septemba, 2020 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles.
Chanzo: tumeyauchaguzi_tanzania (Instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.