WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameitaka Tume ya Utumishi wa Umma kutekeleza mpango mkakati wa kushughulikia rufaa za watumishi wa umma kwa wakati pamoja na kuandaa na kutekeleza mpango mkakati utakaowawezesha waajiri kupunguza ongezeko la mashauri ya kinidhamu yanayowasilishwa Tume ya Utumishi wa Umma kufanyiwa maamuzi.
Mhagama ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma kilicholenga kuhimiza ufanisi wa utendaji kazi wa Tume hiyo.
Mhagama amesema, rufaa zikifanyiwa kazi kwa wakati, Tume itakuwa imetenda haki kwa watumishi wenye mashauri ya kinidhamu, na kuongeza kuwa mashauri ya kinidhamu yasiposhughulikiwa kwa wakati watumishi wanapoteza haki zao na waajiri wanapoteza haki ya kumuadhibu mtumishi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutumishi zilizopo.
“Ushughulikiaji wa rufaa ukifanyika kwa wakati, mtumishi atakuwa ametendewa haki ya kutoadhibiwa anapobainika kutotenda kosa na haki ya kuadhibiwa baada ya kuthibitika kutenda kosa,” Mhagama amesisitiza.
Mhagama ameongeza kuwa, mashauri ya kinidhamu yakichukua muda mrefu, Serikali inaingia gharama kuyaendesha na watumishi wanaokabiliwa na mashauri ya kinidhamu wanakosa tija kiutendaji kwasababu muda mwingi wanautumia kufuatilia mashauri yao badala ya kufanya kazi.
Tume ya Utumishi wa Umma ikitekeleza majukumu yake ipasavyo italisaidia taifa kutenda haki kwa mtumishi wa umma na kuepuka kuingia gharama kubwa ya uendeshaji wa mashauri ya kinidhamu ili kuokoa fedha za umma.
Aidha, Mhagama Tume ya Utumishi wa Umma kwa uamuzi wa kutengeneza mfumo wa ushughulikiaji wa rufaa na malalamiko ambao utakuwa na uwezo wa kuzifikia kwa wakati mamlaka zote za ajira katika utumishi wa umma na kuongeza kuwa, kuwepo kwa mfumo huo ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu na ndio maana amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Tume hiyo kuwezesha mfumo ukamilike kwa wakati
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.