TUME ya Utumishi wa Walimu inajivunia kushughulikia mashauri 8,684 na kuyatolea uamuzi katika kuhakikisha uwajibikaji wa haki na maadili kwa walimu nchini katika kipindi cha miaka mitano ya utendaji kazi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi msaidizi Ajira na maendeleo ya Walimu, kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu, Mectildis Kapinga alipokuwa akielezea mafanikio ya Tume hiyo katika siku ya TAMISEMI maalumu kwa ajili ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma iliyopo jijini hapa.
Kapinga alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji kazi ya tume hiyo imepata mafanikio makubwa katika kukatua kero za walimu. “Tume ya Utumishi wa Walimu tangu kuanza kazi kwake tarehe 1 Julai, 2016, ilikuta kuna mashauri ya walimu mengi ambayo hayajafanyiwa kazi. Mashauri tuliyoyapokea na kuyasajili yalikuwa ni 9,819. Kati ya mashauri hayo, mashauri 8,684 yametolewa uamuzi na mashauri yaliyobaki ndani ya mwaka huu wa fedha tunaamini tutayakamilisha” alisema Kapinga.
Katika kipindi hicho, tume ilipokea na kusajili rufaa za walimu 675, rufaa zilizotolewa uamuzi ni 610, rufaa zilizobaki uamuzi wake utatolewa ndani ya muda mfupi ujao, aliongeza.
Akiongelea ushiriki wa tume hiyo katika siku ya TAMISEMI maalum kwa ajili ya elimu, Mkurugenzi huyo alisema kuwa wapo kwa ajili ya kuwaeleza wadau majukumu ya Tume na kujibu hoja mbalimbali zinazowahudu walimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.