Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inaendelea na mageuzi makubwa katika kilimo cha zao la Zabibu ili kiweze kuinua kipato cha wananchi na kukuza pato la taifa.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akichangia katika mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya jiji.
Mafuru alisema kuwa halmashauri yake inapambana kuhakikisha zao la Zabibu linazidi kukua. “Zao la Zabibu ni kipaumbele chetu, bahati nzuri Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika anafanya kazi nzuri. Tumepeleka wataalam wetu watatu Cape town, Afrika Kusini kujifunza kilimo cha Zabibu. Tumetumia mapato ya ndani kwa wataalam wetu hao kwenda Afrika Kusini kwa siku 10 ili kuleta mapinduzi katika kilimo cha Zabibu” alisema Mafuru.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kuhakikisha zao la Zabibu linashika kasi, alipeleka wachumi kuweka kambi mkoani Morogoro kwa siku 10 kwa ajili ya kuandika maandiko ya miradi ya maendeleo itakayosaidia kukuza zao hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.