Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri ametoa pongezi kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutoa shilingi Bilioni 1.5 kwa vikundi 111, ikiwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mapato yanayopatikana kutoka kwa walipa kodi, sehemu ya mapato hayo 10% inarudi kwa walipakodi kupitia mikopo isiyo na riba.
Pongezi hizo amezitoa katika tukio la utoaji hundi ya mkopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, lililofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
“Nawapongeza viongozi wa Jiji la Dodoma kwa kuridhia kwenye vikao vyao na kutenga fedha kwa ajili ya makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuzitoa fedha hizo kwa asilimia 100 mmefanya jambo jema sana. Ni wajibu wetu kama viongozi kuhakikisha wananchi wanashiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.” alisema Shekimweri.
Aidha, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema katika kuunga mkono ukuzaji na uendelezaji wa uchumi kwa wananchi wa Dodoma, jiji limetenga maeneo kwa ajili ya kuwakopesha wanavikundi ili kutatua changamoto za maeneo ya kufanyia miradi kwa wanavikundi.
“Maeneo yakufanyia kazi imekua changamoto wengi wanafanyia miradi majumbani, namuelekeza Afisa Maendeleo akae na vikundi atuorodheshee vikundi visivyo na maeneo ya kufanyia kazi, jiji lina ardhi yakutosha, kuna viwanja vingi tumepima haitakuwa na maana tugawe kwa watu wengine wakati wa kwetu wanashida” alisema Mafuru.
Akitoa taarifa ya utoaji mikopo ya 10% ya mwezi January hadi April 2022 Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Sigilinda Mdemu amesema kuwa katika mkopo huo vikundi vya Wanawake ni 59, Vijana 44 na Watu wenye ulemavu 8 idadi hiyo inafikisha jumla ya Vikundi 111.
Mgeni rasmi Mhe. Jabir Shekimweri (wa pili kushoto) akikata utepe kwenye tukio la kukabidha hundi ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma, Mhe. Meja (Mst.) Risasi akishuhudia.
Mgeni rasmi Mh. Jabir Shekimweri akimkabidhi mmoja wa vijana pikipiki (bodaboda) kama sehemu ya mikopo ya vikundi vya vijana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.