Aliyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherere za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa Chato, Mkoani Geita.
"Nawapongeza wananchi wa Chato kwa kuwa wenyeji wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021 na kufanikisha kilele cha mbio hizi."
"Mwenge wa uhuru umezindua jumla ya miradi 1,067 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.2."
"Awamu zote zimekuwa zikimuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Kambarage Nyerere."
"Tunawajibika kumuenzi Baba wa Taifa, Mw.Nyerere kwa kuwa alikuwa kiongozi bora, kiongozi asiyewabagua watu na aliwajali wanyonge ambao walikuwa wanahitaji kukombolewa."
"Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisisima imara kupinga ubaguzi hapa nchini na duniani kwa ujumla."
"Serikali itaendeleza na kudumisha falsafa, itikadi na mema yote yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere."
"Vitendo vya rushwa ni chanzo ch kukosekana kwa haki kwenye jamii."
"Miradi 49 imebainika kuwa na kasoro wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru hivyo naagiza wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu huu wachukuliwe hatua."
"Mwalimu Nyerere aliamini kuwa yeye kama kiongozi anahitaji kujenga Taifa linalojitegemea."
"Bila afya bora hatuwezi kuimarisha uchumi wetu, nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya maradhi yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu, hivyo nitoe rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kuzingatia ushauri wa kitaalum."
"Madawa ya kulevya yanaathiri nguvu kazi ya Taifa, hivyo natoa wito kwa vijana kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya."
"Natoa rai kwa vijana kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI."
"Vijana ni injini ya maendeleo ya Taifa na uhai wake."
"Serikali inajipanga kujenga Chuo kikubwa cha TEHAMA hapa Afrika Mashariki na kati kwa kutambua mchango wa sekta hii katika uchumi na kuzalisha ajira."
"Tutaendeleza mambo yote mazuri yaliyoanzishwa na Hayati, Dkt. John Pombe Magufuli yakilenga kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote."
"Serikali inakamilisha vigezo vya kuifanya Wilaya ya Chato kuwa Mkoa."
"Nawakumbusha wananchi wote kuitunza na kuiendeleza miradi yote ya maendeleo iliyozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021."
Chanzo: Idara ya Habari - MAELEZO
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.