Na. Dennis Gondwe, DODOMA
JAMII imetakiwa kufanya suala la usafi kuwa sehemu ya utamaduni ili kuonesha ustaarabu, kujali na kutunza afya.
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kuongea na mamia ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la usafi wa mazingira Kata ya Majengo jijini hapa.
Prof. Mwanfupe alisema kuwa suala la usafi ni ustaarabu na linatakiwa kuwa utashi wa mwananchi mwenyewe.
“Niseme jambo moja kwa wafanyabiashara na wote mliofika hapa kwamba ukiona suala la usafi inabidi litungiwe sheria ujue hiyo jamii inaendelea kufa. Suala la usafi wa mazingira linabidi liwe ni utashi wa mwananchi mwenyewe. Suala la usafi inabidi liwe la kila mmoja na halipaswi kuwekewa Polisi wala kutungiwa sheria ngumu. Lakini pale tunapolazimika kutumia Polisi, tunapolazimika kutumia sheria tujue tunapoenda siyo kuzuri. Kwa sababu kupumua hakuna sheria, kula hakuna sheria, kunywa maji hakuna sheria. Kwa maana hiyo, tuchukulie suala la usafi kama sehemu ya maisha yetu na kamwe tusisubiri kuwa na sheria kali katika suala la usafi wa mazingira” alisema Prof. Mwamfupe.
Awali Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alisema kuwa usafi wa mazingira ni zoezi endelevu kwa jiji hilo na jamii inatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.