Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameshauri miti ya matunda kupandwa katika shule ya sekondari Hombolo Makulu inayojengwa ili kuitikia agenda ya lishe wilayani humo.
Shekimweri alishauri hilo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari Hombolo Makulu.
Shekimweri alisema kuwa eneo la shule hiyo lipandwe miti ya matunda ili kuchochea masuala ya Lishe bora. “Tunataka watoto wakitoka nje wakutane na maua wajifunze kupenda bustani na wajifunze kupenda kupanda miti. Na eneo hili itapandwa miti mchanganyiko hasa ya matunda. Miti hiyo ni kujibu agenda ya lishe wilayani Dodoma. Miti ya matunda, miti ya vivuli na huko kwenye vivuli tuweke na vimeza vya kusomea. Watoto wakipigwa na mitihani wapate hewa safi ya ‘oxygen’ na maarifa ndiyo yataweza kuingia vizuri” alisema Shekimweri.
Alisema kuwa shule nzuri ya aina ile yenye majengo mengi yaliyopangiliwa vizuri haitoshelezi kama haitakuwa na mandhari nzuri. “Tumeshaanza kupanda miti hapa na tutaendelea kuipanda. Baada ya kufanya usafi na leveling hapa, mimi nikuhakikishie hapa tutaweka bustani nzuri” alisema Shekimweri.
Nae mzazi Agatha Kihori alisema kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa masuala ya lishe jambo linaloendea kudumaza hali ya lishe katika kata yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.