Na Josephina Kayugwa, Dodoma
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema Tanzania bila kichaa cha Mbwa inawezekana ikiwa wananchi watajitokeza kuchanja mifugo yao kama Paka na Mbwa wenye dalili na wasio na dalili ya kichaa cha Mbwa ili kuzuia madhara yatokanayo na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
Aliyasema hayo leo tarehe 28 Septemba, 2022 katika maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Mnadani kata ya Mpunguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kauli mbiu isemayo " kichaa cha mbwa, afya moja vifo sifuri".
"Wajibu wetu wa kushiriki katika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambao unaathiri wanyama na binadamu na hauna tiba bali unazuilika kwa kuchanja mbwa na paka.
"kosa kisheria kuacha mbwa na paka wanazurura mitaani bila kuwa na uangalizi, hivyo nitoe wito kwa wananchi wote wanaofuga mbwa kuhakikisha wanazingatia ufugaji bora wa mbwa ikiwa ni pamoja na kutokuwaacha wanazura mitaani," alisema Senyamule.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma za mifugo Prof. Hezron Nongo amesema katika maadhimisho na wiki ya kutoa chanjo ambayo yanaisha tarehe 2 Oktoba, 2022 chanjo ni bure hivyo wananchi wanatakiwa kuwapeleka wanyama wao kupatiwa chanjo ya kichaa cha Mbwa.
"Wananchi wote wa kata ya Mpunguzi pamoja Halmashauri nzima ya Jiji la Dodoma mnatakiwa kutumia fursa hiyo kwa sababu wanyama wengi hawajapata chanjo hiyo ya kichaa cha Mbwa.
"Kuna madhara mengi ambayo yanatokana na ugonjwa huu wa kichaa cha Mbwa lakini pia usalama unakuwa mdogo hata kwa wakazi wa eneo husika hasa watoto wadogo ambao wanaonekana ndio wahanga wa matukio ya kung'atwa na Mbwa kwa kiasi kikubwa, alisema Nongo.
Maadhimisho ya kichaa cha Mbwa duniani hufanyika kila mwaka tarehe 28 Septemba, 2022 kwa kutoa elimu juu kuzuia na kupambana na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa na kutoa chanjo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.