• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ubunifu suluhu ya mapato vyuo vya Maendeleo ya Jamii- Waziri Dkt Gwajima

Imewekwa tarehe: August 24th, 2023

SERIKALI imesema ubunifu wa miradi utasaidia vyuo vya Maendeleo ya Jamii kukusanya mapato zaidi na  kujiendesha kwa kiasi kikubwa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima alipokua akijibu hoja mbele ya  Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa  kikao na Kamati hiyo juu ya uendeshwaji wa chuo cha Maendeleo ya Jamii  Rugemba jijini Dodoma.

Waziri Dkt. Gwajima alisema endapo Vyuo  vya Maendeleo ya Jamii vitaweza kuwekeza katika ubunifu wa miradi mbalimbali itakuwa ni njia ya haraka ya wao kupata pesa ambazo zitawawezesha kujiendesha na kupunguza utegemezi Serikali kuu.

“Tukiwekeza  kwenye miradi yetu kama kilimo,ufugaji na miradi mingine mingi kulingana na eneo husika kwa ubunifu  na ustadi naamini tutaweza kuongeza kipato na kupunguza utegemezi wa fedha kutoka serikalini “alisema Dkt. Gwajima.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu alisema suala la uanagenzi ni jambo linalofanyika katika Vyuo vyote vya Maendeleo ya jamii nchini ili kutoa wataalam wenye ujuzi watakaweza kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya Jamii na Taifa.

“Mbinu ya Uanagenzi inatumika katika vyuo vyote vya Maendeleo ya Jamii  vilivyo chini ya Wizara ikiwa na dhumuni la kuwanoa wanafunzi katika maeneo  muhimu waliojifunza Vyuoni  kwani mafunzo hayo ni zaidi ya mafunzo kwa vitendo maana wanafunzi hupata muda zaidi wa kuweza kuimarika katika eneo  husika.” alisema Dkt. jingu

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq, aliishauri Serikali kushirikiana na wadau tofauti  wa maendeleo kwenye kukuza miradi iliyopo katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili iweze kusaidia katika uendeshaji wa Vyuo hivyo.

“Ili miradi hii ikue  ni vyema  mkitumia mbinu ikiwemo kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo waasisi wa chuo hiki waliokuwa na lengo la kusaidia watoto wa kike. Njia hii inaweza kuchochea mafanikio makubwa na yenye uendelevu” alisema Toufiq

Sambamba na hilo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ilipitishwa kwenye wasilisho la mfumo wa Kidigitali wa taarifa wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambao umetengenezwa ili kuleta uwazi na uwajibikaji kwa wadau wote  wa NGOs nchini.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.