Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza rasmi siku ya Jumatano ya tarehe 28 Oktoba, 2020 kuwa siku ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara ikitanguliwa na ratiba ya uteuzi wa wagombea na kampeni.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage, amesema Uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Ubunge, na Udiwani utafanyika tarehe 25 Agosti, 2020 na Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 26 Agosti, 2020 hadi 27 Oktoba, 2020.
Amesema Tume imetoa taarifa hiyo chini ya Ibara ya 41(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na vifungu vya 35B (1), (37) (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 48 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
"Tume inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa Ratiba ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara itakuwa kama ifuatavyo. Uteuzi wa Wagombea Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Ubunge, na Udiwani utafanyika tarehe 25 Agosti, 2020, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 26 Agosti, 2020 hadi 27 Oktoba mwaka huu wa 2020 na Siku ya Uchaguzi itakuwa tarehe 28 Oktoba, 2020" amesema Jaji Rufaa (Mst) Kaijage.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage alipokuwa akitangaza ratiba ya uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles wakiwa kwenye bango la Uchaguzi baada ya mwenykiti kutangaza ratiba ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles waakiondoa pazia kufungua bango la Uchaguzi baada ya kutangazwa kwa ratiba ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam leo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.