ZOEZI la upigaji kura uchaguzi wa Serikali za mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma limefanyika katika hali ya amani na usalama likishughudia mamia ya wananchi wakijitokeza.
Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alipokuwa akiongea baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura jijini hapa leo.
Kimaro amesema kuwa zoezi la upigaji kura kwa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilianza saa moja asubuhi na kumalizika saa 10 jioni kwa mujibu wa kanuzi za uchaguzi huo. “Vifaa vyote vilifika vituoni kwa wakati na wananchi wamehamasika na kujitokeza kuwapigia kura viongozi wanaowapenda” alisema Kimaro.
Akiongelea hali ya usalama katika zoezi hilo, Kimaro alisema kuwa zoezi hilo limefanyika katika hali ya amani na utumivu. “Hali ya ulinzi na usalama ilikuwa shwari, Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma ametimiza wajibu wake wa kikanuni wa kudumisha ulinzi na usalama katika vituo vyote” alisisitiza Kimaro.
Zoezi linaloendelea ni la kuhesabu kura zilizopigwa na matokeo yatatangazwa leo jioni baada ya zoezi kukamilika. “Matokeo yatatangazwa leo hii na yatabandikwa kwenye vituo husika vya upigaji kura” alisema msimamizi huyo.
Katika hatua nyingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo amelidhishwa na zoezi la upigaji kura lililofanyika katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Mhe Jafo alipata nafasi ya kutembelea vituo vya Chihikwi na Chadulu ‘B’ na kuridhishwa na zoezi linavyoendelea” alisema msimamizi huyo.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina mitaa 222, mitaa 220 wagombea wake walipita bila kupingwa. Mitaa ya Chihikwi kaya ya Mbalawala na Chadulu ‘B’ kata ya makole ndiyo ilifanya uchaguzi ikihusisha vyama viwili, Chama cha Mapinduzi (CCM) na chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.