Na. Dennis Gondwe, DODOMA
UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma unafanyika kwa uwazi kwa mujibu wa kanuni zilizopo ili wananchi wafurahie kukua kwa demokrasia.
Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwenendo na shughuli mbalimbali za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazoendelea ofisini kwake leo.
Dkt. Sagamiko alisema kuwa hakuna mpango wowote wenye nia ovu ya kuminya demokrasia kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa. Alisema kuwa tangu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaanza ulikuwa wa wazi na shirikishi ukiruhusu vyama vyote kushiriki kikamilifu.
Akiongelea zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi alisema kuwa vyama vyote 19 vilishiriki zoezi hilo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Halmashauri ya Jiji la Dodoma tunajivunia mafanikio haya ya kidemokrasia. Vyama 15 ndivyo vimechukua na kurudisha fomu kwa nafasi mbalimbali za uongozi” alisema Dkt. Sagamiko.
Akiongelea upotoshaji unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mipango inayopangwa kuengua baadhi ya wagombea kutoka moja ya chama cha siasa alisema kuwa hakuna mipango hiyo. Alisema kuwa hakuna uteuzi wa wagombea uliofanyika hadi itakapofika tarehe 8 Novemba, 2024. Aidha, aliwata wananchi kuwapuuza wale wote wanaotaka kuleta taharuki katika jamii kwa kutoa taarifa za upotoshaji. “Sisi kwa umoja wetu, siyo tu tuzipuuze taarifa hizo za upotoshaji bali kuendelea kutoa elimu. Kuendelea kuwasisitiza wananchi kufuata kalenda ya matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa uwazi ilibandika orodha ya wapiga kura ili watu waweze kuhakiki usahihi wa taarifa hizo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.