MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewahakikishia wananchi wa Ihumwa juu ya utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara inayoanzia barabara kuu iendayo Dar es salaam mpaka stesheni ya Treni ya mwendokasi (SGR) kwakuwa ni sehemu ya miradi itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/24.
Mavunde ameyasema hayo tarehe 27/05/2023 wakati akiwahutubia wananchi wa Ihumwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Ihumwa ukitanguliwa na zoezi la uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ihumwa.
“Tunamshukuru sana Mh. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya miundombinu Jijini Dodoma ambayo ina lengo la kuliboresha Jiji ya Dodoma.
Barabara hii ipo kwenye kitabu cha bajeti cha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika ukurasa wa 247 kasma 4230 ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya dhati ya serikali kuujenga mradi huu ili kutatua adha ya barabara kwa wananchi wa Ihumwa” Alisema Mavunde.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya Cde. Charles Mamba amewataka viongozi wote wachaguliwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kutatua kero za msingi za wananchi.
Akitoa maelekezo ya awali, Diwani wa Kata ya Ihumwa Mh. Edward Magawa ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kwa na ushirikino wa Mbunge Mavunde kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ambayo yataibadilisha kata ya Ihumwa kwa kiasi kikubwa na kuwataka wananchi wampe ushirikiano katika kuwatumikia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.