UJENZI wa awamu ya kwanza jengo la kitega uchumi linalojengwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mji wa Serikali 'Government City Complex' limefikia asilimia 65 ya ukamilikaji.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkandarasi anayejenga mradi huo kampuni ya Mohammed Builders wakati wa ukaguzi uliofanywa na wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Januari 18, 2021 ni kwamba, ujenzi huo wa awamu ya kwanza unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu.
Wajumbe wa kamati hiyo ya Fedha wakiongozwa na Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Emmanuel Chibago walielezea kuridhishwa kwao na maendeleo ya mradi huo huku wakimuagiza mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
Mradi huo unajengwa na Jiji katika Mji wa Serikali Mtumba kwa kutumia mapato ya ndani kwa gharama ya shilingi bilioni 56 hadi kukamilika kwake, ambapo utakuwa na hoteli, taasisi mbalimbali kama benki, maduka makubwa, Migahawa, makazi (Appertments), kumbi kubwa tatu kwa ajili ya mikutano mbalimbali, ambapo pia Jiji hilo linakamilisha ujenzi wa hoteli ya ghoroga 11 iliyofikia asilimia 98 ya ukamilishaji, ujenzi huo pia unatumia mapato ya ndani ya Halmashauri inayojulikana kama Dodoma City Hotel yenye vyumba 105 ikiwa katikati ya Jiji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.