SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) imeanza ujenzi wa daraja la Chipogoro Wilayani Mpwapwa katika barabara itokayo Dodoma kwenda Iringa litakalogharimu kiasi cha shilingi Milioni 601. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge katikati ya wiki hii amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa kijiji cha Chipogoro, vijiji vya jirani na watumiaji wa barabara ya Dodoma - Iringa. Kumalizika kwa daraja hilo kutaondoa kero ya mafuriko wakati wa kipindi cha masika katika eneo hilo.
Daraja hilo linajengwa eneo ambalo limekuwa likituamisha maji mengi na kusababisha mafuriko nyakati za msimu wa mvua jambo ambalo lilihitaji kuwa na daraja litakalowezesha maji kupita bila kutuama.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.