• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu wafikia 98%

Imewekwa tarehe: January 25th, 2025

Na. Dennis Gondwe, ZUZU

UJENZI wa Kituo cha Afya Zuzu umefikia asilimia 98 ya utekelezaji kikitarajiwa kuhudumia wananchi 10,054 kwa kuwahakikishia huduma bora za afya na kuwaondolea hadha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Goodluck Magoti alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Magoti alisema “kutokana na changamoto ya kukosa huduma za Kituo cha Afya katika Kata ya Zuzu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilianza ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu ili kusogeza huduma za matibabu mbalimbali karibu na wananchi. Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi 299,439,348,54. Hadi kufikia sasa kiasi cha shilingi 285,4439,000,54 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara na kubakiwa na shilingi 14,000,348.54 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi. Ujenzi umefikia asilimia 98 ukiwa katika hatua ya umaliziaji”.

Akiongelea faida za mradi huo alisema kuwa utakapokamilika utasaidia watu 10,054 kupata huduma za afya. “Kuwapunguzia akina mama wajawazito umbali mrefu wa kupata huduma za kujifungua. Kusogeza karibu na jamii huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali” alisema Magoti.

Kwa upande wa kiongozi wa ‘route’ namba mbili Naibu Meya, Fadhili Chibago alipongeza na kusema kuwa kazi iliyofanyika ni nzuri. “Niwashauri kuwa muandae halfa ya uzinduzi wa kituo hiki ili wakazi wa Kata ya Zuzu na vitongoji vyake wafahamu mchango wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa maendeleo yao ambazo ni kodi zao” alisema Chibago.

Nae Diwani wa Kata ya Miyuji, Beatrice Ngerangera alisema kuwa tukio la uzinduzi wa kituo hicho iwe kumbukumbu ya kihistoria. “Nashauri katika uzinduzi huo uambatane na tukio la kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu. Pia Mheshimiwa Mizengo Pinda ashirikishwe katika tukio hilo kwa sababu ni mkazi wa kata hii” alisema Ngerangera.

Ikumbukwe kuwa Kata ya Zuzu ilianza kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya tarehe 15 Agosti, 2022 kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukitekelezwa kupitia mfumo wa ‘force account’ awamu ya kwanza mradi ukihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, maabara na kichomea taka.

MWISHO

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.