• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ujenzi wa SGR waendelea kwa kasi, Trilioni 2.957 zatumika hadi sasa

Imewekwa tarehe: March 3rd, 2020

Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.957 kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) huku kasi ya utekelezaji ikiongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaendelea kama ulivyopangwa.

“Mradi wa SGR kwa kipande cha Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia asilimia 75 wakati kipande cha Morogoro Makutopora Singida kimefikia takribani asilimia 28”, Alisisitiza Dkt. Abbasi

Akifafanua Dkt. Abbasi amesema kuwa watanzania wataanza kutumia usafiri huo wa kisasa kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro mwaka huu wa 2020 hivyo ile ahadi ya Serikali kwa wananchi itatimia kama ilivyopangwa na kwa wakati.

Kwa upande wa kipande cha Mwanza-Isaka Dkt. Abbasi amesema kuwa wakati wowote zabuni itatangazwa ili kumpata mkandarasi atakayejenga reli hiyo kwa kipande hicho ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwezi Desemba 2019 Jijini Mwanza kwa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumzia baadhi ya wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi kama SGR Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa hata wanaobeza watanufaika na miradi hiyo ikiwemo ndege na umeme.

Kwa upande wa utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP), ujenzi wa eneo la kuchepusha maji ya mto Rufiji ili ujenzi wa ukuta wa bwawa uanze limekamilika kwa asilimia mia moja. Aidha bwawa hilo linatajwa kuwa kati ya mabwawa makubwa 70 ya kuzalisha umeme wa maji Duniani na kwa Afrika litakuwa la nne kwa ukubwa.

Kwa upande wa kiwango cha fedha kilicholipwa hadi sasa Dkt. Abbasi amesema kuwa Shilingi Trilioni 1.275 kati ya Trilioni 6.5 zimeshalipwa ambapo kazi zote zinaendelea kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara zote wametembelea mradi wa SGR ili kujionea utekelezaji wake.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa Chelezo katika Ziwa Victoria Dkt. Abbasi amesema kuwa umekamilika kwa asilimia 100 na Shilingi Bilioni 32.8 zimeshalipwa na katikati ya mwezi Machi itaanza kufanya kazi, huku ukarabati wa MV Victoria umefikia asilimia 89 na Bilioni 14 zimeshalipwa. Wakati MV Butiama ukarabati wake umefikia asilimia 86 na Bilioni 3 zimeshalipwa kati ya Bilioni 4 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo.

“ Ujenzi wa meli mpya na ya kisasa katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na Tani 400 za mizigo umefikia asilimia 52 hadi sasa na unaendelea kutekelezwa kwa kasi kama ilivyopangwa.

Utaratibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali kukutana na vyombo vya habari unalenga kuileta Serikali kwa pamoja na wananchi kwa kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maslahi yao katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Chanzo: www.maelezo.go.tz - Msemaji Mkuu wa Serikali

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.