UJUMBE maalum ulioongozwa na Madiwani Mhe. Msinta Mayaoyao wa Kata ya Majengo na Mhe. Neema Mwaluko wa Kata ya Kilimani, uliojumuisha wajumbe Mkufya Msekeni Mwanasheria wa Jiji la Dodoma pamoja na Wataalama washauri kutoka Engage Consult wametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya ili kujifunza na kupata uzoefu wa uundaji na uendeshaji wa Chombo cha kisheria chenye lengo maalum (Special Purpose Vehicle - SPV) kinachotarajiwa kuundwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Ujumbe huo ukiwa Jijini Mbeya ulipata nafasi ya kuonana na viongozi vya Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiwemo madiwani na wataalam wa Jiji hilo miongoni mwao ni Mweka Hazina na Mchumi wa Jiji hilo.
Halmashauri ya Jii la Dodoma inakusudia kuunda chombo hicho kitakachokuwa na mali na dhamana ya kisheria ili kisimamie na kuendesha miradi ya vitegauchumi vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usalama wa kifedha bila kuingiliwa au kuathiliwa na hali ya kifedha ya mmiliki yaani Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.