WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani upimwe kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo.
"Sisi tunataka tuone makusanyo ya mapato yetu yakusanywe kwenye vyanzo vyote vizuri zaidi ili tuende kupeleka kwenye miradi. Tujenge miradi, ujenzi wa miradi kwa mapato ya ndani kigezo hicho ni kizuri zaidi. Kigezo cha madaraja ni rahisi watu kuweka makadirio ya chini ili waweze kukusanya mapato na kuvuka malengo ili waibuke kidedea". amefafanua Waziri Mkuu.
Aidha, amewataka Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kusimamia jambo hilo. Akifafanua zaidi Mhe. Majaliwa amesema Halmashauri nyingi pamoja na makusanya zaidi ya asilimia hatujaona mradi hata mmoja wa kimkakati unaokumbukwa kwa makusanyo hayo.
Vilevile, ametoa mfano wa baadhi ya Halmashauri ambazo zinakusanya hadi Bilioni 28 lakini ukienda hata mradi wa Milioni 500 haupo! "Tunataka tuone Halmashauri zinashindana kujenga miradi kutokana na mapato yenu, mapato ya Serikali kuu iwe ni ziada". amesema Mhe. Kassimu Majaliwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.