WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amezielekeza halmashauri zote nchini kuwa na miundombinu bora ya kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka ili kulinda afya za wananchi.
Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo leo Januari 6, 2021 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika soko la Majengo Jijini Dodoma kwa lengo ni kuangalia mfumo mzima wa ukusanyaji, uhifadhi na usafirishaji taka.
Akifafanua Waziri amesema, sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake inazitaka halmashauri za manispaa, wilaya, miji na majiji kuweka mfumo bora wa kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka.
“Nimefurahi kuona Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameweka mfumo mzuri na miundombinu bora ya kuhakikisha kwamba taka ngumu zinakusanywa na kusafirishwa kupelekwa dampo, na bahati nzuri nimeuliza wanawake hawa (waliokuwa karibu) na wamenihakikishia kwamba taka hazikai zaidi ya siku moja,
Nitumie fursa hii kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji, uhifadhi na usafirishaji taka” amesema Waziri.
Aidha, Waziri Ummy amesema hii ni mwanzo, angetamani kuona wanaboresha zaidi na pia ametumia fursa hiyo kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kwanza wanakuwa na miundombinu bora ya kuhifadhi, kukusanya na kusafirisha taka, akitolea mfano wa Jiji la Dodoma ambao wana gari na wana vizimba vinavyotumika kukusanyia taka, pili amesema ni kuhakikisha pale ambapo halmashauri wanapotoa kandarasi kwa watu wa kukusanya na kusafirika taka, watu hao wawe na vifaa bora.
Vilevile, amesema utafanyika ukaguzi kwa kila halmashauri wajitathmini kuhusu kandarasi walizotoa kwa ajili ya kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka kama wana vifaa bora, watumishi wenye vigezo, sifa na kama wana vifaa vya kuwakinga watumishi wanaokusanya taka.
Tunataka masoko yetu yawe safi na salama kwa wanaouza na wananchi wanaofika sokoni kupata mahitaji yao ya kila siku.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.