NAIBU Meya wa Halmashauri ya jiji la Dodoma Emmanuel Chibago amesema tatizo la upungufu wa madarasa katika Halmashauri hiyo litamalizwa kufikia katikati ya mwezi Februari kutokana na mkakati na juhudi zinazofanywa katika kujenga madarasa mapya ili wanafunzi wote wanaopaswa kuanza kidato cha kwanza waanze masomo mara moja.
Aliyasema wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hususan ujenzi wa madarasa mapya uliofanywa na wajumbe wa Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika shule kadhaa ambapo wajumbe hao walielezea kuridhishwa na na nkasi ya ujenzi na ubora wa majengo.
“Kwa spidi ambayo tunaiona nafikiri mpaka tarehe 15 mwezi wa pili tutakuwa tumekamilisha na tarehe 28 watoto wataingia madarasani bila kukosa” alisisitiza Naibu Meya Chibago.
Aliwashukuru wasimamizi na wadau mbalimbali wa miradi hiyo wakiwemo watendaji wa Kata na walimu kwa ushirikiano na usimamizi wa karibu katika kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika kwa wakati.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.