Utaratibu wa kufanya usafi kila Jumamosi kwa wananchi wa Jiji la Dodoma uliendelea wiki hii karika maeneo mbalimbali ya Jiji.
Akizungumza baada ya kumalizika zoezi la usafi katika Kituo cha Afya Mkonze, Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu Dickson Kimaro aliwapongeza wananchi waliojitokeza kushiriki kufanya usafi katika kituo cha afya.
Kimaro alisema, "nimefurahishwa mno na jinsi watu wa Mkonze mlivyoitikia na kuja kushiriki zoezi hili muhimu la kusafisha na kuweka mazingira ya kituo chetu cha afya kuwa vizuri".
Kituo cha Afya Mkonze kwa muda sasa kimekuwa kikifanyiwa maboresho kwa kuongeza baadhi ya majengo mapya ya kutolea huduma kama vile maabara, wodi ya watoto, chuma cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi. Hivyo ilikuwa ni muhimu kushiriki kwa pamoja kuweka mazingira ya kituo katika hali ya usafi wakati shufhuli za ujenzi zikielekea mwishoni.
Aidha, Kimaro aliwasihi wananchi wa Jiji la Dodoma kuendelea kujitokeza kwa wingi karika maeneo yao ya makazi, biashara na shughuli mbalimbali kufanya usafi umbali wa mita 5. Akasisitiza kuwa Jiji limeweka muda mzuri wa kila mwananchi kushiriki kila Jumamosi kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi. "Ndugu zangu mjue kuwa wakati wa muda wa kufanya usadi, shughuli zote za biashara yakiwepo maduka, vibanda, na biashara zozote zinatakiwa kuwa zimedungwa ili kuroa nafasi kwa kila mtu kushiriki kazi ya usadi" alisema Kimaro.
Wananchi wa Mkonze wakishiriki kufanya usafi.
Usafi ni jukumu la kila mwananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.